Header Ads

MAJANGA FULL VIDEO 300 WAFARIKI DUNIA KWA KUFUNIKWA NA KIFUSI

Rais Ernest Koroma wa Sierra Leone ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kwa wahanga waliofariki kutokana na maporomoko ya udongo yaliyotokea Jumatatu pembezoni mwa mji wa Freetown. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais, maombolezo ya kitaifa yataanza tarehe 16 hadi 22 mwezi huu, ambapo bendera zote zitapepea nusu mlingoti. Wizara ya habari ya nchi hiyo imesema idadi ya wahanga waliofariki katika janga hilo imefikia 297, wakiwemo watoto 109, wanawake 83 na wanaume 105, na kazi ya uokoaji bado inaendelea.Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.