Header Ads

Makubwa...Msanii Ruby Akana Ujauzito Wake...Picha Zanaswa Zikionyesha Ushahidi
Akifanya mahojiano na EATV, Rubby amesema kwamba watanzania wengi wanapenda kufuatilia masuala ya watu hata kama kiasi kwamba haawatamani baadhi ya mambo mengine yawapite hata kama na kuongeza hata kama anaweka mitandaoni ni mambo yake binafsi na yanapaswa kuachwa.

"Mimi sijawahi kusema kama nina ujauzito mahali popote lakini wabongo wamelishadadia sana suala hili ambalo mimi nimejiwekea tu mtandaoni..... Wameaanza kuniita sasa hivi mama K na mimi nimelikubali jina hilo na moja kwa moja najiita mama K kama wanavyotaka. Siwezi kusema kama nina ujauzito lakini kwa sasa nina-focus zaidi kwenye muziki wangu..... kwani nina project nyingi za kufanya kwa wakati huu. Isitoshe nina kazi ya kuachia mwezi huu wa nane" amesema Rubby.

Mbali na hayo Rubby amedai hakukaa kimya bure amekuwa anafanya mambo ya msingi na  mwezi wa nane  watu watajua ni kitu gani kilimkalisha kimya.

"Nilikuwa kimya kwa sababu kuna mambo mengine yalinipelekea kukaa kimya japo sitapenda kuyazungumzia kwa sasa. Hata hivyo kama msanii nilikuwa nafanya kazi zangu maana msanii napaswa kuwa na nyimbo nyingi na hilo nimelifanya lakini mwezi wa nane nitaachia video pamoja na audio kwa pamoja nadhani litakuwa jibu la ukimya wangu. aliongeza Rubby.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.