Header Ads

Mke wa Roma Awapa Makavu Wale Wanaosema Safari ya Zimbambwe ya Mke wa Mume ni Kiki

Mke wa Roma Awapa Makavu Wale Wanaosema Safari ya Zimbambwe ya Mke wa Mume ni Kiki
Mke wa rapa Roma Mkatoliki, bibie Nancy Mshana amedai watu wanaodhani mume wake katumia kiki ya kwenda Zimbabwe ili wimbo wake mpya uwe gumzo wapo sahihi na hafikirii kumlaumu mtu yeyote kwani ni uhuru wa kujieleza

 Nancy amesema kuwa hafahamu kama mumewe anaweza  kumtumia  kama kupata kiki na iwapo kama ni kweli  mume wake kafanya hivyo  basi kafanikiwa kwa kiasi kikubwa  atakuwa ametisha
"Watu kama wanadai hii ni kiki ni idea nzuri sana kwani katumia njia sahihi. Pia mimi naona ni jambo zuri kama amenichagua mimi na ameona hii ndiyo njia sahihi ya ya kukuza muziki wake mimi ninamsapoti kwani siku zote nimekuwa nikimsapoti katika kazi zake ambazo zinatufanya chakula kifike mezani.

Akizungumzia maisha ya umaarufu Nancy anasema bado hajaona kama yana ugumu kwani yeye hajawa mtu wa kujichanganya sana katika makundi ya watu, kitu ambacho anamuomba Mungu kisije kikabadilika na kumbadilishia mfumo mzima wa maisha yakle.
Hata hivyo mwana mama huyo alikataa kuweka wazi ni kitu gani kilichompeleka Zimbabwe mume wake

"Safari yake ilikuwa ya ghafla sana na hajakwenda kufanya show. Lakini mimi sipendi kuweka wazi kwani nitaharibu 'suprise' iliyoandaliwa lakini yeye akirudi atawaambia kila kitu, sitaki kuharibu suprise mapema.

Pamoja na hayo Msanii Roma amewashawasili nchini usiku wa kuamkia jana kutoka Zimbabwe ili kuanza 'Media tour' ya wimbo wake mpya 'Zimbabwe' uliokuwa gumzo kila kona ya mji kutokana na mashairi yake.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.