Header Ads

Shilole Aishukia Ndoa ya Nuh Mziwanda...Adai Wapambane na Hali yao

Shilole Aishukia Ndoa ya Nuh Mziwanda...Adai Wapambane na Hali yao

KUTOKANA na kuwepo kwa madai ya Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kuchangia kuvunjika kwa ndoa ya mpenzi wake wa zamani, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, msanii huyo wa muziki na filamu ameibuka na kusema mambo hayo hayamhusu.

Vyanzo mbalimbali kwa nyakati tofauti vimedai kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi baina ya wapenzi hao wa zamani licha ya Nuh kuwa katika ndoa, kitu kilichokuza mgogoro wa wanandoa hao ambao wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kike, kiasi cha mwanamke kuamua kutimka.

Baada ya kupata habari hizo, Za Motomoto News ilimtafuta Shilole ambaye alijibu kwa kifupi; “Kila mtu apambane na uhusiano wake, pia mambo ya ndoa kuvunjika hayanihusu.”

Naye Nuh akasema; “Migogoro ndani ya ndoa ni kitu cha kawaida, kuhusu Shilole siyo kweli, Nawal alikuwa na mambo yake hivyo alikuwa anatafuta kisingizio cha kuondoka, sijampa talaka bali aliamua kuondoka mwenyewe hivyo ninachoweza kusema ni kwamba namshukuru Mungu ninaendelea kupumua hayo mengine ni ya ziada tu, kikubwa uhai.”

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.