Header Ads

Watu Zaidi ya 50 Wanusurika Kifo kwa Ajari ya Basi la Kampuni ya Saibaba

Watu Zaidi ya 50 Wanusurika Kifo kwa Ajari ya Basi la Kampuni ya Saibaba
Abiria zaidi ya hamsini wamenusurika kifo baada ya basi la abiria la kampuni ya Saibaba aina ya scania lenye namba za usajili T 131 AZZ likitokea Dar es Salam kwenda Sumbawanga, kuacha njia na kupinduka eneo la Chimala wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Mohammed Mpinga, amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 1:20 usiku Agosti 27 mwaka huu na kusababisha majeruhi watano waliolazwa kwenye hosptali ya Chimala mkoani Mbeya.

Kamanda Mpinga amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo Hussein Mkwizu(52) mkazi wa jijini Dar es Salaam, alipojaribu kulipita lori na ndipo basi likapoteza mwelekeo na kupinduka.

Pia Kamanda Mpinga ametoa wito kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani, na kwamba Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.