Header Ads

Bob Junior Awapa Makavu Wanaoingilia Beef Lake na Diamondi Asema Awajui Undani wa Tatizo

Bob Junior Awapa Makavu Wanaoingilia Beef Lake na Diamondi Asema Awajui Undani wa Tatizo
Aliyekuwa producer wa Diamond Platnumz ambaye pia ni msanii wa Bongo Flava, Bob Junior amewataka mashabiki kuliacha kama lilivyo suala lake na Diamond kwani hakuna anayejua mwanzo wa kazi zao.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Give Me’ ameiambia Bongo Dot Home ya Times Fm kuwa mashabiki wanaingilia kitu wasichokijua kiundani kitu ambacho si sawa.

“Ukweli ni kwamba hawapaswi kunizungumzia na yeye kwa sababu wakati tulikuwa tunatengenezana tulikuwa wawili, kwa hiyo huwezi kuingilia wewe kama shabiki maandazi kwa kuingilia vitu ambavyo huvijui.

“Mimi na yeye tulikuwa tunafahamiana wakati tupo chumbani, katika chumba cha studio lakini bada ya hapo tukawa wakubwa, sasa wewe shabiki ambaye unazungumza unamjua yeye? au unanijua mimi?, au mimi na yeye ndio tunajuana zaidi?,” amesema.

Ameongeza kuwa, “kwa hiyo wewe unaingia kati baada ya kumfahamu Bob Junior na huyo muhusika (Diamond), unaanza kumtetea yeye au kunitukana mimi wakati sisi hatuwafamu”.

Bob Junior amekuwa akimshutumu Diamond kwa kutangaza kuwa kuna kolabo ambayo wangefanya pamoja lakini hakuna utekelezaji na anapomtafuta ili kuzungumzia hilo amekuwa akimpuuza.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.