Header Ads

Breaking News: Nyumba ya Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma, yaungua moto


Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe aliyoijenga  wakati akigombea ubunge kwa mara ya kwanza  iliyopo Kibingo, Kata ya Mwandiga mjini Kigoma imeungua moto jioni hii.

Nyumba hiyo iko kiwanja kimoja na nyumba yake ya sasa imeteketea yote na chanzo chake hakijafahamika hadi sasa.

Msaidizi wa mbunge huyo, Nyembo Mustafa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hata hivyo Zitto hakuwa anaishi kwenye nyumba hiyo.

Amesema Zitto alihama kwenye nyumba hiyo baada ya kujenga nyumba nyingine kubwa kwenye kiwanja hicho hicho na iliyoungua ilikuwa ikitumika kwa dharura.
TOA MAONI YAKO

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.