Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Gambo Atoa Ushauri Kuhusu Kufukuzwa Kazi

Gambo Atoa Ushauri Kuhusu Kufukuzwa Kazi

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo ametumia ukurasa wa Facebook kuwapa nguvu vijana na kuwafariji juu ya mambo mbalimbali ambayo yanatokea katika maisha na kusema kuwa vijana wengine wanaona hawawezi jambo fulani ni kutokana na kuwa na njia mbadala.


Mrisho Gambo amesema kuwa katika maisha ya kawaida siku ambayo mtu akifukuzwa kazi ndipo anaweza kugundua kuwa anaweza kuishi maisha yake vizuri bila ya kuwa na hiyo kazi na siku ambayo vijana wengine wanaweza kuanza kutumia vipaji vyao watagundua kuwa wanaweza kuishi bila kutegemea vyeti vyao.
"Siku utakayofukuzwa kazi utashangaa kuwa unaweza kuishi bila hiyo kazi, siku utakayoanza kutumia kipaji chako utashangaa kuwa unaweza ishi bila Digrii yako, siku Utakayoanza kutumia Ubunifu au Kutumia Taaluma yako utagundua kuwa unaweza kuishi bila kutegemea kupandishwa cheo, mengi unayodhani huyawezi ni kwa sababu tu una njia mbadala" alisema Mrisho Gambo
Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.