Header Ads

VIDEO: LADY JAY DEE ''WABONGO TUNASHOBOKEA SANA WA NJE''
Msanii Wa Bongo Flava,Lady Jay Dee Amesema Wabongo Tuna Shobokea Sana Wa Nje,Kauli Hiyo Ameiongea Kupitia Kipindi Cha The Finest Kinachorushwa na A.FM 92.9 kuanzia Juma Tatu Mpaka Ijumaa,Saa Sita Mchana Mpaka Saa Tisa Alasiri Kupitia Watangazaji Wake Winsto Makangale,Daniella Ngenzi Na Dj Wao Dj Massu.

Lady Jay Dee Amesema,Madj Na Mapresenter wa Tanzania, Wanapiga sana nyimbo za nje kuliko za bongo,na pia Wasanii wa Tanzania wamekuwa Wanafuata upepo ulipo katika kazi zao,Ikija Style ya Nigeria wanaimba kama nigeria,ikija ya south wanaimba kama south,hivyo bongo flava haijui identity yake ni ipi.

Akiongea kupitia kipindi cha Kijiweni katika mahojiano aliyofanya na watangazi wa kipindi hicho Ally Mohamed na Aggness Anderson Lady Jay Dee amesema hataki mazoea na watu asiowajua na ndio mana watu wengi wamekuwa wakisema kuwa anaringa ila si kweli.

Jay Dee ameongeza kuwa yeye sio muongeaji na huwa ni vigumu  sana kwake kupiga mastory na mtu ambaye hajamzoea,japo salamu anatoa.

 Hata hivyo kwa mara nyingine tena mwanadada huyu atafanya vitu vyake akiwa na mpenzi wake Spicy and the band Siku ya leo Eid mosi ndani ya kiota kipya cha Burudani Dodoma Capetown Kisasa,akisindikizwa na mkali wa singeli Msaga Sumu na Nay wa MitegoGet it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.