Header Ads

Lulu Diva Akanusha Kujichubua Afunguka Mboga Mboga Zinavyo Badirisha Ngozi Yake

Lulu Diva Akanusha Kujichubua Afunguka Mboga Mboga Zinavyo Badirisha Ngozi YakeMsanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma ya 'Give it to me', Lulu Diva amekanusha zile tuhuma za yeye kujichubua ngozi yake na kudai kinachofanya aonekane kuwa mweupe ni kutokana na kula mboga za majani na matunda kwa sana.

Lulu Diva ameeleza hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo kutoka East Africa Radio baada ya watu wengi kuanza kumuoneshea vidole kuwa anajipiga kitaulo (anajichubua) kwa maana rangi yake ya awali haikuwa hivyo.
"Unajua kwamba msanii unatakiwa uanze kujitengeneza mwenyewe kuanzia mwili wako, ngozi pamoja na vitu unavyokula. Naweza sema nakula sana mboga mboga na matunda, kuna baadhi ya vyakula vinasaidia hata kung'arisha ngozi", amesema Lulu Diva

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.