Header Ads

Maskini...Yusuph Manji Yupo hoi, Ashindwa Kufika Kortini


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kusikiliza utetezi katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabishara Yusuf Manji baada ya kuelezwa kuwa anaumwa.

Wakili wa mshitakiwa, Hajra Mungula alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa kesi imekuja kwa ajili ya utetezi lakini wamepata taarifa kuwa mshitakiwa hajafika. Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 8 mwaka huu kwa ajili ya utetezi. Mahakama hiyo ilitakiwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo jana kwa upande wa utetezi ambapo tayari shahidi mmoja ameshatoa ushahidi wake.

Wakati huo huo, katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Manji na wenzake watatu, imeahirishwa hadi Septemba 8, mwaka huu kwa sababu hiyo hiyo. Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43), mkazi wa Chanika wanakabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi.

Wakili wa Serikali, Paul Kadushi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mshitakiwa Manji anaumwa na kwamba upelelezi haujakamilika lakini wanaendelea kusisitiza upelelezi ukamilishwe.

Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 8 mwaka huu. Inadaiwa Juni 30, mwaka huuu maeneo ya Chang’ombe A wilayani Temeke Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja, walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vyenye thamani ya Sh milioni 192.5.

Pia inadaiwa Julai mosi mwaka huu, maeneo ya Chang’ombe A, wilayani Temeke, Dar es Salaam, washitakiwa wote walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo nane ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za JWTZ vyenye thamani ya Sh milioni 44. Katika mashitaka ya tatu, inadaiwa Juni 30, mwaka huu maeneo ya Chang’ombe A, washitakiwa walikutwa wakiwa na mhuri wa JWTZ ambao uliandikwa ‘’Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha JWTZ’’ bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama wan chi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.