Powered by Blogger.
[4] [Tech] [slider-top] [Technology]

Latest Post

HABARI KALI ZA WIKI

[15] [recent] [slider-top] [HABARI KALI ZA WIKI]

Technology

Lifestyle

HABARI ZA BURUDANI

[4] [burudani] [recent] [HABARI ZA BURUDANI]

Sports

VIDEO KALI ZA WIKI

NEW SONG:DIAMOND FT A,K,A

Gallery

Random Posts

Business

Boss Ngasa

Boss Ngasa

Video Of Day

STORI KALI ZA WIKI

[5] [habarimbalimbali] [recent] [STORI KALI ZA WIKI]

Popular Posts

Pages

STAY CONNECTED

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]

CONTACT US

SIASA

[4] [siasa] [recent] [HABARI ZA SIASA]

Flicker Images

TUMA UDAKU PICHA AU VIDEO KUPITIA 0716909567

Facebook

About US

Advertisements

Entertainment

Follow US

You are here: Home / Rais Magufuli Amwapisha Ibrahim Juma kuwa Jaji Mkuu

Rais Magufuli Amwapisha Ibrahim Juma kuwa Jaji Mkuu

| No comment


Rais Magufuli Amwapisha Ibrahim Juma kuwa Jaji Mkuu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amemuapisha Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alimteua kushika wadhifa huo Septemba 10, mwaka huu (Jumapili).


Katika ghafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa wakiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Majaji wengine wa Tanzania, Jaji Ibrahim Juma aliyeapishwa amesema anashukuru kwa kurasimishwa kushika wadhifa huo, ambao alikuwa ana ukaimu takriban miezi nane mpaka alipoteuliwa kuwa Jaji Mkuu.

Katika hotuba yake ya kwanza Jaji Mkuu Ibrahi Juma ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa weledi ikiwemo kulinda sheria na kuweka imani kwa wananchi, kwani wao ndiyo watetezi wao.

"Jambo ambalo ni muhimu kwetu sisi katika kufanya kazi ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwa na imani ya wananchi, kwa sababu wananchi wasipokuwa na imani na Mahakama pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama hawatakuja kwetu ili kutatua matatizo yao. Sisi tumejiwekea mipango ya kuhakikisha tunaendelea kupata imani ya wananchi wetu, na tutafanya hivyo kwa kuepuka utovu wa maadili, vitendo vya rushwa na ucheleweshaji wa mashauri", amesema Jaji Mkuu Ibrahim Juma.

Ibrahim Juma alianza kutumikia wadhifa wa Kaimu Jaji Mkuu tokea Januari 18 mwaka 2017, baada ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa nchi Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kustaafu.