Header Ads

Wolper Atoa Somo Kuhusu Watu Wenye Lengo la Kumshusha Mtu Kimaendeleo

Wolper Atoa Somo Kuhusu Watu Wenye Lengo la Kumshusha Mtu Kimaendeleo


Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameanza kuwa mshauri wa mambo kadhaa katika maisha ya kila siku.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, mrembo huyo ametoa ushauri juu ya baadhi ya binadamu wanaotaka kumshusha mtu kimaendeleo na kutaka kumkwamisha pindi wakimuona na furaha.

"Basi leo nataka niwaambie kitu hakuna binadamu anaependa hivyo ww ulivyo na ndio maana unakuta wanazua mambo mengi ili wajaribu kukufanya ujione mdhaifu,Binadam bwana wanaweza wakatafuta tatizo pasipo kuwa na tatizo!Wakiona mtu yupo happy anajitafutia,anafanya yanayo muhusu wanaona hilo ni kosa na mbaya zaidi wakigundua una furaha wanajaribu kukufanya uwe down,Ingawa sio wote lkn wapo hawa watu na wengine tupo nao majumbani mwetu tunaishi nao..Unakuta mtu unafanya kitu kizuuuri lkn haupongezwi kwa lolote mbaya zaidi wanakiponda ili ujikatie tamaa na hiyo yote kwasababu wao hawana basi wanataka ww uwe km wao…Sasa niwashauri ndugu zangu tusiwe watu wakuchulia kitu km kilivyo kuna wengine wanataka kukuona tu umeshindwa hiyo ndo furaha yao wao,fanya mwenyewe,amua mwenyewe na pia jipongeze mwenyewe ikiwezekana nyamaza kabisa wasijue yako ila wape nafasi ya kuona mafanikio yako..Usikubali kumpa mtu mwingine nafasi zaidi ya ww unavyotakiwa kujipa..Jipe nafasi,Jipongeze na jiamini bila kujali mwingine anasema au atasema nn…Pambana na uwezo wako cha msingi usishindane nao…Amini unaweza kupitia wewe mwenyewe!

Kwa sasa mrembo huyo amejikita katika biashara ya mavazi na duka lake limekuwa likitengeneza nguo kwa kuzishona.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.