Header Ads

Kidato cha Nne Kuanza Mtiani ya Taifa Kesho

Kidato cha  Nne Kuanza Mtiani ya Taifa Kesho


Mitihani ya Taifa kidato cha nne hapa nchini inatarajiwa kufanyika siku ya kesho nchi nzima ambapo watahiniwa 385,938 wanatarajiwa kufanya nchini.

Hyo yamesemwa leo, Oktoba 29,2017 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde .

Dk Msonde amesema mtihani huo utaanza kesho Oktoba 30,2017 hadi Novemba 17,2017 huku  maandalizi ya mitihani yameshakamilika.

Amezitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unafuatwa.

Katibu mtendaji huyo amewataka wanafunzi kuacha vitendo vya udanganyifu wakati wa kufanya mitihani kwa kuwa wanaweza kufaulu bila kufanya hivyo.

Dk Msonde ametoa onyo kwa wasimamizi na wanafunzi  watakaojihusisha na udanganyifu na kusema kuwa baraza hilo halitasita kuwafutia mitihani wote.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.