Header Ads

NIMEKUWEKEA PICHA NA VIDEO YA TUNDU LISSU LEO AKIWA ANAFANYA MAZOEZI NA KUONGEA NA WATANZANIA LEO


Dar es Salaam. Kwa mara ya kwanza, picha ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) imeonekana hadharani baada ya kuwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) tangu Septembea 7.

Lissu ameonekana leo Jumatano kupitia picha akiwa amekaa katika kitanda cha Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Katika picha hizo, Lissu anaonekana akiwa mwenye tabasamu huku akiwa amepunga mkono kuashiria kuwasalimu ndugu, jamaa na marafiki zake.

Picha hizo zimekuwa gumzo katika mitandao mbalimbali ya kijamii na zimekuwa zikisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii.

Jana Jumanne, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe aliwaambia waandishi wa habari kuwa hali ya Lissu inaendelea vizuri na kwamba picha zake za video zingetolewa wakati wowote


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.