Header Ads

Uongozi wa Mlimani City Waeleza Sababu ya Kuifungia NakumattUongozi wa Mlimani City umelifungia duka kubwa (Supermarket) la Nakumatt tawi la Mlimani City Jijini Dar es salaam kutokana na kutotimiza majukumu yake kama mlipakodi wa jengo hilo hivyo kurudisha nyuma upatikanaji wa Mapato.

Meneja mkuu wa Mlimani City, Pastory Mrosso ameeleza kwamba wamechukua hatua hiyo baada ya uongozi wa Nakumatt kutotekeleza wajibu wake wa kulipa kodi kama mpangaji kwa muda mrefu.

Hatua hiyo uya kufuingiwa kwa duka hilo kumezua taharuki na mshtuko kwa wafanyakazi walioajiriwa humo kwani wengi wao wameeleza kuwa hawakuwa na tarifa zozote na bado wanadai stahiki zao.

Wafanyakazi hao walikuwa wamezongana nje ya lango kuu la kuingilia katika duka hilo wakiwa na taharuki pasipo kujua hatma yao baada ya kufungiwa kwa duka hilo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.