Wema Sepetu Ataja Sababu Zilizomfanya Asiende Kumuona Tundu Liss
Mrembo
wa Tanzania na Kada wa Chadema Wema Sepetu ametoa ya Moyoni kwa nini
hakwenda kumuona mapema Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu baada ya
kupigwa risasi septemba 7 ni kwamba asingeweza kumuona akiwa kwenye
maumivu.
Wema
ameweka wazi maneno hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni
baada ya dakika chache tangu kuachiwa kwa picha za kwanza za Mbunge huyo
akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Wema
ameandika "Kisichokuua kinakufanya uwe na nguvuz zaidi....Utarudi tena
ukiwa na nguvu kuliko ulivyokuwa awali...Shujaa wetu. ... Picha hii
imenifanya nipate hisia. Sasa naweza andaa safari ya Nairobi kuja
kukuona.. Awali nisingeweza kuvumilia kukuona ukiwa kwenye maumivu".
Wema
Sepetu ametajwa na Chama cha Chadema kama mmoja wa wahamasishaji
aliyeweza kuhamasisha watu kutoa michango kwa ajili ya matibabu ya
Mbunge Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa
risasi na watu wasiojulikana alipokuwa kwenye gari lake nje ya makazi
yuke huko mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment