Header Ads

Ali Kiba Awaacha Watu Njia Panda Awaachia Swali Hili Mashabiki " Nini Kinafuata?"

Ali Kiba Awaacha Watu Njia Panda Awaachia Swali Hili Mashabiki " Nini Kinafuata?"


Staa wa muziki wa bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ ameanza kuonesha dalili za ujio wa kazi nyingine baada ya ‘Seduce Me’ iliyoingia kwenye rekodi ya kazi zake zilizopokelewa vizuri zaidi ndani ya muda muda mfupi kwa mwaka 2017.

AliKiba sio mtu wa maneno mengi katika kuachia kazi zaidi ya vionjo vya kugusia gusia kwa maneno machache ya kinachopatikana katika kazi yake yoyote pindi anapoelekea kuiachia rasmi ambapo mapema leo aliweka picha yake akiuliza mashabiki kuwa nini ‘Kinafuata?? ‘What Next…?.
Muda mfupi baadae mara baada ya post hiyo iliyoambatana na swali, Kiba aliweka picha yake nyingine akiwa na muongozaji wa video mpya ya kolabo ya wimbo ‘Malo’ wa Tiwa Savage uliyowashirikisha StarBoy ‘Wizkid’ na Spellz, Director Meji Alabi. Swali likaibuka Je’ anachouliziwa kuwa nini kifuate kimeongozwa na Director Meji Alabi ambaye aliongoza video ya hitsong ya ‘Chekecha Cheketua’ ya AliKiba.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.