Header Ads

Beka Awachana Gigy Money, Shilole 'Wanatafuta Kiki Tu'

Beka Awachana Gigy Money, Shilole


 
 
HASIMU wa muziki wa Aslaya Isihaka, mkali wa ngoma ya Libebe, Bakari Katuti ‘Beka Flavor’ amewachana wasanii wenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’, kwa kujikweza kuwa wanatupia ‘vitu’ vya gharama kali wakati si kweli.

Beka ameifungukia Full Shangwe hivi karibuni baada ya Shilole kujitapa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ametupia ving’aro vyenye thamani ya Sh. milioni kumi, huku Gigy Money naye akijinadi kwa kusema kuwa, wigi lake ni la Sh. milioni sita!

“Hamna cha mamilioni yoyote zaidi ya kutengeneza tu kiki, wasanii wana mbwembwe sana, wengine wanadanganya wana mali nyingi wakati si kweli. Mimi siwezi kufeki uhalisia wa maisha yangu na siwezi kuendesha muziki kwa kutegemea kiki kwa sababu najiamini kwa kazi zangu,” alisema.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.