Header Ads

Lema Amtondoa Wasiwasi Mange Kimambi "Mange,Nimekusoma Maamuzi ya Dhati Yatatoka kwa Wananchi Usiogope"

Lema Amtondoa Wasiwasi Mange Kimambi "Mange,Nimekusoma Maamuzi ya Dhati Yatatoka kwa Wananchi Usiogope"Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amemtoa wasiwasi mwanadada anayefahamika kama mwanaharakati wa mitandaoni Bi. Mange Kimambi kuwa asijali kwani wananchi watatoa maamuzi juu ya kilichotokea kwenye uchaguzi mdogo Jumapili iliyopita.

Lema amelazimika kumuondoa wasiwasi mwanadada huyo baada ya kuonyesha hisia za hasira kwaviongozi wa upinzani ambao wamekuwa wakilalamika kufanyiwa madhamibi na Chama Cha Mapinduzi huku akiwataka wachukue maamuzi magumu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange amemwambia lema "Haki mnawachosha wananchi. Mpaka mnaonekana masnitch yani kama vile mnatumika na CCM. We need stronger leadership than this. Chukueni maamuzi magumu acheni kulia lia kama wajane..Mnafanya mpaka mtu unatamani kuwatukana"
Baada ya Maoni marefu Mange aliyoyaandika, Lema amemjibub Mange kwa kumwambia;
"Mange,nimekusoma/ nimekuelewa watu wana hasira kuhusu mambo yanoyoendelea nchini hususani ktk uchaguzi huu wa marudio ya udiwani,  kelele juu ya dhuluma hizi ni muhimu, acheni kwanza watu wote wajue kilio chetu, . Only Time will tell. Usiogope" Lema.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.