Header Ads

VIDEO:Inasikitisha Boss Amhamuru Mfanyakazi Wake Kutembea Uchi Ofisini

Inasikitisha Boss Amhamuru Mfanyakazi Wake Kutembea Uchi Ofisini
Yaani unaambiwa dunia ina mambo kweli kweli kwani tumesikia mengi na tutaendelea kushuhudia mengi zaidi. Boss mmoja mjini Warsaw, nchini Poland ameamuru mfanyakazi wake mmoja wa kike kutembea uchi ndani ya Ofisi kubwa ya mauzo ya jumla ili kuongeza molali na ufanisi kazini kwa wanaume ambao alidai kuwa wamekosa ari kwenye utendaji.

Mwanamke huyo ambaye naye hakuwa na namna alivua nguo zake zote huku akiziba kifua kwa sidiria na kutumia mawani ya jua na kuanza kutembea ofisini mbele ya Wanaume waliokuwa wamesimama msururu kwa amri kutoka kwa Boss.
Taarifa kutoka kwa vyombo vya habari nchini Poland, vimeeleza kuwa mwanamke huyo alilipwa pesa mara tatu ya mshahara wake ili kufanya tukio hilo kwa lengo la kuwachangamsha wanaume ili kurudisha ari ya utendaji kazi.

Hata hivyo tukio hilo lilifanyika kwa muda wa dakika 20 tu na baadae mwanamke huyo akavaa nguo na kukaa kwenye meza yake na kuendelea na majukumu yake kazini hapo kama kawaida.Tazama video hapa chini (Video by Daily Mail)

Video hiyo inayoonekana imerekodiwa kwa kutumia simu ilianza kusambaa mtandaoni nchini humo wiki iliyopita huku watu wengi wakipinga vitendo kama hivyo mitandaoni na kumkosoa Boss wa Kampuni hiyo ya mauzo. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.