Header Ads

Ajiokoa Kwenye Ajali ya Moto juu ya Ghorofa kwa Kuning’inia Dirishani (Video)


Mwanaume mmoja nchini China amejikuta akiokoka kwenye moto mkubwa uliozuka kwenye jengo refu lenye ghorofa 25 kwa kuvunja vioo na kuning’nia dirishani bila kudondoka.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la Chongqing Daily zimeeleza kuwa moto hupo ulianza kuwaka leo Jumatano Desemba 13, 2017, Mnamo majira ya 05:55 asubuhi ambapo moto huo ulianzia ghorofa namba 24 kuelekea ghorofa namba 25 ambayo yeye ndiye aliyekuwepo.

Kwa muonekano wa video iliyorekodiwa kwa kutumia simu, Mwanaume huyo alionekana akining’inia kwenye madirisha na baadaye kushuka floo ya chini baada ya moto kuongezeka.

Akiwa katika jitihada za kujiokoa alionekana akivunja vioo kwenye ghorofa ya chini ambayo ilikuwa bado haijapatwa na moto huku akidondokewa na vipande vya makaa ya moto kutoka juu.

Hata haikumgharimu muda mrefu kupata mateso hayo kwani baada ya dakika 9 yaani saa 06:04mchana  kikosi hicho cha Moto cha mjini Yuzhong kilifika na kufanikiwa kuuzima moto huo na kuwaokoa watu watatu akiwemo mwanaume huyo.

“Tulifika muda mfupi baada ya kutokea kwa moto, tuliagiza maaskari wetu 71 kuzima moto huo lakini ilitulazimu kwanza kumuokoa mwanaume mmoja aliyekuwa nje ya jengo hilo akihangaika kujinasua na moto. Maaskari wetu walilazimika kuvunja madirisha kwa mashine zetu, lakini tulikuta watu wawili ndani ya jengo hilo wakiwa wameungua vibaya na kuwapeleka hospitali.“imeeleza taarifa ya kikosi cha zima moto cha mjini Yuzhong.

Hata hivyo majina ya majeruhi wote watatu bado hayajulikana kwa sababu za kiusalama nchini humo. Tazama kipande cha video cha tukio hilo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.