Header Ads

Huu Hapa Ushauri wa Rais Magufuli Kwa Wale Vyuma Vilivyokaza “Vyuma Vimekaza na Bado Vitavunjika Kabisa, Nawashauri Muweke Grisi,”

Huu Hapa Ushauri wa Rais Magufuli Kwa Wale Vyuma Vilivyokaza “Vyuma Vimekaza na Bado Vitavunjika Kabisa, Nawashauri Muweke Grisi,”


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John P. Magufuli amewajibu watu wanaolalamika vyuma vimekaza kwa kuwambia kuwa vyuma vikikaza vinatakiwa kuwekwa grisi vilainike, vinginevyo vitavunjika kabisa.

Rais Magufuli amesema kuwa watu wote wanaolalamika kuwa maisha magumu na hela hazi0nekani ni watu waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali ndiyo maana wanalalamika vyuma vimekaza.

“Vyuma vimekaza na bado vitavunjika kabisa, nawashauri muweke grisi,”amesema Rais Magufuli leo Alhamisi Desemba 14,2017 mjini Dodoma kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewataka Walimu wote nchini watakaohamishwa bila kupewa pesa za uhamisho kukataa kuhama hadi watakapopewa pesa hizo kwani kitendo hicho hakiwezi kuwafukuzisha kazi.

“Usihame kama hujalipwa pesa yako, hakuna atakayekufukuza kazi kama hajakulipa pesa ya uhamisho,”amesema Rais Magufuli.

Soma zaidi hotuba yake yote – Mambo 31 aliyozungumza Rais Magufuli wakati akifungua mkutano Mkuu wa chama cha Walim

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.