Header Ads

Jacqueline Wolper Ametia Aibu ya Mwaka kwa Mashabiki Wake

Jacqueline Wolper Ametia Aibu ya Mwaka kwa Mashabiki WakeSTAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ametia aibu ya mwaka mbele ya mashabiki wake wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa (birthday) kufuatia gauni alilovaa ambalo lilishindwa kumstiri maumbile yake nyeti, Ijumaa Wikienda lilikuwepo.

Tukio hilo la aina yake lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Buckets uliopo Masaki jijini Dar ambapo katika sherehe hiyo mbali na pati hiyo pia alizindua ‘App’ yake ambayo atakuwa akiweka kazi zake zote za sanaa pamoja na biashara zake huku akipewa sapoti na mastaa wengi wakiwemo Steve Nyerere, Gigy Money, Amber Lulu, Barnaba, Aunt Ezekiel na wengine kibao.

Akizungumzia shughuli yake hiyo, Wolper aliwashukuru mashabiki wake waliohudhuria akisema: “Asanteni kwa wote mliokuja kunipa sapoti kwenye siku yangu hii.

“Nilizaliwa Desemba 6, nil­isherehekea na watoto yatima.
“Lakini leo (usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita), nimeamua kusherehekea pamoja nanyi mashabiki wangu. “Naombeni muendelee kuniunga mkono pia kwenye App yangu ambayo nimeizindua leo.”

Hata hivyo, mbali na sham­rashamra hizo, jambo lililo­geuka gumzo kubwa ni gauni alilovaa mwanadada huyo.
Gauni hilo lilikuwa jeusi ambalo liliacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi hasa katika maungo yake ya mbele kiasi kwamba alionekana kwamba kwa ndani alikuwa ametinga ‘kufuli’ pekee.

Kufuatia hali hiyo, muda mwingi Wolper alionekana aki­jitahidi kujiziba eneo la mbele kwa viganja vya mikono, jambo lililowafanya baadhi ya watu kuhoji kwamba kama alikuwa akiona aibu alivyovaa nusu utupu basi asingevaa hivyo!
“Sasa anafichaficha nini? Si amevaa mwenyewe? Kwa nini asiachie tu watu tuone vitu….” Alisikika jamaa mmoja aliyeonekana kudata baada ya kujionea ‘vitu’ vya ndani ya Wolper.

Hata hivyo, mbali na wengi kuonekana kuliponda gauni hilo matata, wapo waliolisifia kwamba ni mkali wa mitindo.
Chanzo: Global Publishers

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.