Header Ads

Mc Pilipili Avutiwa na Nafasi ya Ben Pol kwa Ebitoke

Mc Pilipili Avutiwa na Nafasi ya Ben Pol kwa EbitokeMchekeshaji Mc Pilipili ameizungumzia style aliyoitumia mchekeshaji mwenzie, Ebitoke hadi kuingia katika mahusiano na Ben Pol.

Mc Pilipili amesema Ebitoke ni mchekeshaji mzuri sana ila style aliyoitumia kumuendea Ben Pol pengine kwa nia ya kutangaza jina lake angeweza kufanya kazi zaidi kama mbadala wake.

“Bado kuna ombwe limeingia Tanzania kwamba inabidi uwe na kiki fulani halafu ndio unaleta kazi zako lakini mimi bado naamini kazi ina nguvu zaidi, hayo mambo tuachie waimbaji” Mc Pili ameiambia Bongo5.

Alipoulizwa iwapo yeye angekuwa Ben Pol angelichukuliaje hilo, alijibu; “(anacheka) ni ngumu, kwanza unajua Ben Pol ni mgogo mwenzangu na nina uhakika walikuwa na mipango yao mizuri na kuna sehemu waliishia, wapo poa”.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.