Header Ads

Nuh Mziwanda Ajibu Mapigo kwa Shilole Picha Zake Akiwa Ndani ya Huba Zito na Pretty Zanaswa

Nuh Mziwanda Ajibu Mapigo kwa Shilole Picha Zake Akiwa Ndani ya Huba Zito na Pretty Kind Picha Zao zza Kimahaba ZanaswaMWANAMUZIKI anayefanya poa Bongo, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kuolewa naye ameijibu ndoa hiyo kwa kujiweka kwa msanii wa filamu za Kibongo ambaye pia anakuja kwa kasi kwenye anga za muziki, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ ambapo picha zao za kimahaba zimenaswa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na wawili hao kilivujisha picha hizo na kueleza kuwa, wawili hao kwa sasa wapo kwenye dimbwi zito la mahaba, kwani mwanadada huyo kafa kaoza kwa baba Anya ambaye ni mzazi mwenziye na Nawal waliyemwagana baada ya ndoa yao ya Kiislamu kuvunjika.
“Hizo picha nilizibamba kwenye simu ya mtu, nikaona siyo mbaya niwape ubuyu wambea wenzangu, habari ndiyo hiyo, Pretty na Nuh sasa mambo ni moto, mbona siyo siri hata huko mitandaoni wanajiachia kwa post za kimahaba.
“Si unajua Shilole kaolewa? Jambo hilo limechangia pia Nuh kuamua kuuweka moyo wake kwa Pretty ili asiumie sana kwani ni mwanamke ambaye alimpenda sana” aliongeza Baada ya kuzinyaka picha hizo zinazowaonyesha wawili hao wakiwa wamepozi kimahaba paparazi wetu alianza kumvutia waya Nuh ambaye simu yake iliita bila kupokelewa, kwa upande wake Pretty Kind alipotafutwa alistaajabu shushushu wetu kuzinasa picha hizo na kuomba apigiwe baadaye.
Baada ya muda alipotafutwa alikuwa na haya ya kusema; “Nuh ni mpenzi wangu ndiyo, sioni tatizo katika hilo, nampenda na yeye naamini ananipenda, kwa kipindi kirefu nimekuwa nikimmezea mate hatimaye sasa amekuwa wangu.”

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.