Header Ads

Wema Aweka Wazi Mahusiano Yake na RC Makonda

Wema Aweka Wazi Mahusiano Yake na RC MakondaTangu mrembo Wema Sepetu akamatwe kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya kwa kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mnamo mwezi Februari mwaka huu, Mrembo huyo hajawahi kumposti wala kumzungumzia kwa lolote kama alivyokuwa akifanya hivyo kipindi cha nyuma.

Watu wengi waliamini kuwa kitendo cha Wema Sepetu kutajwa na RC Makonda kwenye  orodha ya Wasanii waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya kuliondoa urafiki wao waliokuwa nao awali.Sasa, Wema Sepetu ameamua kuwaonesha mashabiki wake kuwa hayo yote yameshaisha na kwa sasa amerudisha yake ya urafiki na RC Makonda kama ilivyokuwa zamani.

Hayo, ameyathibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka picha akiwa na RC Makonda na kuandika kuwa “Kila lenye mwanzo lazima mwisho uwepo“.
Hatua hiyo ya Wema Sepetu imeonekana kuwafurahisha mashabiki wake wengi wakimsapoti kwa maamuzi hayo. Pitia baadhi ya maoni ya mashabiki wake baada ya uamuzi huo

irenefaith_muganda-Safi sana wema wangu safi mno….
hobokelamesson-Duuuuh, kwani kuna ubaya? Watu mapovuu tatizo nini? Safi Sana mdogo angu Wema kuishi vizuri na watu ni hazina, kiroho safi kabisa.
anastaziarug-Huyu ndo wema niliekuwa namutamani mungu akupe kila lililo jema mamy umekuwa sasa
sharifa15-Ni makosa mengi tunafanya hapa duniani lkn MUNGU anatusamehe, sa cha ajabu nn watu wanao fahamiana vzr kusameheana! Mi sijaona kosa.. Madam fanya lile linalo kupendeza km kusema walimwengu hawajaanza leo kukusema.
cynthiajustin-75% of Kenyans got your back. We endorse your decision. God bless @wemasepetu
Kwa upande mwingine, mrembo Wema Sepetu bado anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi na kesi yake itasikilizwa alhamisi ya tarehe 14 Desemba, 2017. kunako mahakama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.