Header Ads

BREAKING NEWS: Scorpion Ahukumiwa Kwenda Jela

BREAKING NEWS: Scorpion Ahukumiwa Kwenda Jela
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemhukumu mwalimu wa sanaa ya kujihami, ‘Martial Arts’ na msanii wa filamu za kibongo, Salum Njwete maarufu Scorpion miaka 7 jela kwa kosa la kumjeruhi na kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho, pia mahakama imemtaka kulipa faini ya TSH. Milioni 30 kwa ajili ya fidia kwa majeruhi huyo.

Kwa upande wake, mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni majeruhi, Said Mrisho amelia mahakamani hapo akidai adhabu aliyopewa Scorpion haitoshi ikilinganishwa na kosa alilotenda huku akieleza kuwa atakwenda kwa Rais Dkt. John Magufuli kumueleza masikitiko yake.

 Njwete anlikuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni  unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Said Mrisho kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo, tumboni na mabegani na kisha kumtoboa macho kitendo anachodaiwa kutenda Septemba 6, mwaka jana  katika eneo  la Buguruni Sheli, jijini Dar es Salaam. Pia, anadaiwa kumwibia mali yenye thamani ya Sh 476,000/-. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.