Header Ads

Diva Amwagwa Dadharani na Heri Muziki Mbele ya Watangazaji Wenzie, Ataka Kuzimia


Yule binti ambaye mahari yake hadi sasa ni Tsh Million 200 za kitanzania na ambaye ni mtangazaji mwenye mvuto kuliko wote hapa Tanzania leo amefanyiwa suprise ya nguvu na aliyekuwa mpenzi wake anayeitwa Heri Muziki.

Diva alimanusura azimie maana kijana wake amemkana wazi wazi mbele ya watangazaji wenzie jambo ambalo Cute Diva hakutarajia kabisa kwani yeye alitarajia kwenda kutambulishwa hadharani na kwa jamii...
Diva alishamgharamikia sana huyu kijana kwani amemtafutia collabo nyingi na amekuwa akimlipia studio sessions kila leo.....akamkutanisha hadi na Mr paul bila kusahau kumpigia nyimbo zake kila leo kwenye kipindi chake cha jioni.....

Pia huyu kijana inasemekana ameshauriwa amwage Diva baada ya kuanza kufeli kwenye masomo yake pale chuo kikuu......

Pamoja na Diva kutumia mbinu ya kumponda GK kuwa hakuwa romantic bado kijana huyu hakushawishika kabisa na kuamua kumkana Diva hadharani tena mbele ya watangazaji wenzake na kibaya zaidi Diva ndiye iliyeomba interview.....

Kwakweli nimemuonea sana huruma Binti malinzi kwakweli alichofanya mtoto Heri sicha kiungwana kabisa japo ni wazi kabisa si vizuri mtu mzima kucheza na watoto....

Lemutuz na Diva huu si mwezi mzuri kwao

Baada ya kukanwa hadharani Binti Diva amesema yafuatayo:

Divatheebawse "Najua napata simu nyingi ila mtanisamehe sana kwa sasa naomba nisiongee chochote kulinda Brand yangu na jina langu.
Interviews zote nikitulia ntawajibu ....
Samahani kwa yoyote aliekwazika...mashabiki. wafanyakaz wenzangu na ndugu jamaa na marafiki!!
Haya ni maisha tu ... "

"Ni ngumu sana kuwa na mahusiano na mvulana uliyepishana naye umri, wanasumbua sometimes"

Divatheebawse "JAMAN naona mnaumia na mimi ..mnapaza sauti mnalia na mimi mko hapa kwa ajili yangu nasema asanteni sana kwa mapenzi mnayoonyesha kwangu wakati wa kipindi hiki cha majaribio .. mapito kipindi cha huzuni kwangu .... niseme tu nimedhalilishwa...nimefedheheshwa....nimeumia sana sana sana!!
Yalionikuta ... sikuhisi yangenikuta ... moyo wangu unasononeka sana! Ndio maana sina ata maneno sahihi ya kusema Namuachia mungu pekee yeye anajua...this is a heartbreak! Afu anaekufanyia hivyo yan ni mtu ambae umejitoa extra kwa ajili yake! Sitasema lolote baya . Namuachia Mungu Yaan sijui ata what to do! ..ndio mana sipokei simu sijibu sms za mtu yan i jus wanna handle this kama mwanamke shupavu mwenye nguvu na mwanamke anaejitambua.
ila nimeumia sana !!

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.