Header Ads

Dudu Baya Amtupia Dongo Jux "Mimi Sio Msanii wa Kulia Lia Kama Jux Anayemlilia Vanessa"


Msanii Dudu Baya amesema kuwa yeye sio msanii wa kulia lia kama Jux anayemlilia Vanessa.

Akiongea  na Planet Bongo ya East  Afrika Radio, Dudu Baya amesema yeye ni msanii anayebadilika kila wakati kulingana na kile kitu mashabiki wake wanataka.

"Mimi nabadilika kila wakati kulingana na mazingira, na ndo maana  ukisikia nyimbo zangu kwa sasa ni kwaajili ya masela na sio watu wa kulia lia, kama wapo watu wanaotaka kulia lia wakamsikilize Jux anayemlilia Vanessa maana sio kila mtu kaachwa na Vanessa," amesema Dudubaya.

Dudubaya ni msanii wa Bongo Fleva aliyetamba zaidi katika miaka ya 2005  na nyimbo zake tofauti ikiwemo mpenzi, nakupenda tu na nyinginezo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.