Header Ads

Kuna Wakati Unatakiwa Ushindwe ili Ushinde – Ruby

Kuna Wakati Unatakiwa Ushindwe ili Ushinde – Ruby
Msanii wa muziki Bongo, Ruby ameamua kuwatia moyo watu ambao wamekata tamaa na vitu wanavyovifanya.

Mrembo huyo mwenye sauti adimu ametoa rahi hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuwaandikia ujumbe usomekao ‘Sometimes you gottaloose to win again #jesusdidit #TZBIRD🇹🇿 #mwakawamaajabu’ ujumbe huu umekuja ikiwa ni siku chache kupita
tokea kuachiwa kwa video mtandaoni ikimwonyesha akiimba wimbo wa kumshukuru mungu uitwao

‘Sitabaki Kama Nilivyo’ wa Joel Lwaga, ambapo mashabiki walimpa moyo na kumwambia kuwa ni msanii mweny kipaji cha utofauti.

Sio hao tu bali hata Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mh. Paul Makonda aliweka video hiyo na kuandikia ‘Mchukue huyu Yesu uone kama kuna mtu wa kukuzuia watajaribu lakini hawatafanikiwa ,hatimaye watajiunga na wewe. Y because you become unstoppable’, wengine ni Meneja wa kundila Tip Top Connection Babu Tale.

Ruby amewahi kuavhia ngoma kama ‘ Na Yule’, ‘Forever’, ‘Sijutii’ na nyinginezo. Pia ameshafanya kazi na wasinii kama Abdu Kiba, Baraka The Prince, Wakazi na wengineo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.