Header Ads

Pretty Kind Amtaka Nuh Mziwanda Kuacha Kutapatapa na Wanamke wa Mjini

Pretty Kind Amtaka Nuh Mziwanda  Kuacha Kutapatapa na Wanamke wa Mjini


MSANII wa filamu za Kibongo ambaye alikuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amemtaka mwanaume huyo atulie na aache kutapatapa na wanawake wa mjini.

Akizungumza na Za Motomoto News, Pretty alisema Nuh anatakiwa aache kutapatapa na wanawake wa mjini na ajikite katika kufanya kazi na kuachana na kutegemea kuhongwa na wanawake.

“Niliachana na Nuh maana nilishindwa kuwa na mwanaume ambaye anataka nimlee wakati nami ndiyo natafuta maisha, namshauri atulie sasa afanye kazi atafika mbali sana kuliko kutegemea kuhongwa,” alisema Pretty.

Nuh alipotafutwa kuhusu ishu hiyo, simu yake iliita bila kupokelewa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.