Header Ads

Sakata la Kiria Kudai Kupigwa na Mumewe: Haya Machozi Namlilia Mungu

Sakata la Kiria Kudai Kupigwa na Mumewe: Haya Machozi Namlilia Mungu
MWANAHARAKATI na masuala ya wanawake nchini Tanzania, Joyce Kiria ameweka hadharani kuwa mahusiano yake na mumewe Henry Kileo ambaye amewahi kuwa kiongozi na Mgombea Ubunge ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Mwanga, Kilimanjaro kuwa hayapo sawa.Kiria amesema mahusiano yao hayapo sawa kwani yeye amekuwa ndiye baba na mama wa familia ikiwa ni pamoja na kuihudumia familia nzima na kumhudumia mumewe huyo.Kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akibubujikwa na majozi, Kiria amededai huwa anamshauri mumewe atafute japo kazi itakayowaingizia kipato ili kusaidiana kutunza familia lakini mumewe amekuwa mkali na kumshushia kipigo.


“Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanyua kunipiga (@kilewo2020mwanga) ukasahau kabisa! ukasahau yooote. Nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote, Malipo yako ni kunipiga/ kunidhalilisha na kunitoa machozi, umenipiga kwa sababu Mimi ni mnyonge siyo! sina nguvu, kwa sababu ni MWANAMKE Sina nguvu za kupigana na MWANAUME.

“Umeniumiza mwili wangu unauma kila mahali, ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ni nini? kuniua??,“ameandika Kiria huku akielezea jinsi alivyompigania mumewe hadi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 hadi akaingiza deni kubwa na kufungiwa kipindi chake cha Wanawake Live kilichokuwa kinaruka EATV.“Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua, kama ni mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto wako kwa miaka yote Mungu yupo. Leo umenipiga (@kilewo2020mwanga)?? Sawa watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu, badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni mwanaume kwa kunipiga.“amemaliza Kiria. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.