Header Ads

Trump Kushindana na Oprah Winfrey Kugombania Nafasi ya Urais 2020

Trump Kushindana na Oprah Winfrey Kugombania Nafasi ya Urais 2020


Rais Donald Trump anasema kuwa ''itakuwa furaha'' kutetea wadhfa wake wa urais dhidi ya aliyekuwa nyota wa kipindi cha mazungumzo nchini Marekani Oprah Winfrey huku kukiwa na wito wa yeye kuzindua kampeni ya kuwania urais.

''Ndio nitamshinda Oprah'', bwana Trump aliwaambia maripota wakati wa mkutano kujadili mabadiliko ya sheria za uhamiaji na maseneta wa Marekani.

Mwanawe wa kike Ivanka Trump alijiunga na raia wengine wa taifa hilo kusifu hotuba ya Oprah wakati wa tuyo za Golden Globe.

Mwandani wa Winfrey anasema muigizaji huyo 'havutiwi' na uwezekano wa kutangaza kuwania urais 2020.

Hotuba yake kuhusu umuhimu wa kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia ilivutia pongezi kutoka kila eneo la Marekani.

Alikuwa na Trump na familia yake. Nampenda sana Oprah lakini sidhani kwamba atawania urais.Nilimjua sana, aliongezea.

Miongo miwili iliopita katika CNN, bwana Trump alisema kwamba iwapo atawania urais basi atamchagua bi Winfrey kuwa mgombea mwenza .''Oprah. Nampenda Oprah''.

''Oprah atakuwa chaguo langu la kwanza'', alimwambia mtangazaji Larry King mwaka 1999.

''Iwapo atawania itakuwa vyema.Ni mtu maarufu, ni mtu mwenye kipaji na mwanamke mzuri sana''

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.