Header Ads

Watu 2,624 Waathirika na Mafuriko Dodoma

Dodoma. Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia amewaomba watu wa kada mbalimbali kutoa msaada kwa wananchi wa kata ya Mrijo mkoa wa Dodoma walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza na waandishi wa habari bungeni leo Januari 17, 2018, Nkamia amesema jana wananchi wengine 161 wamekosa makazi kutokana na nyumba zao kuzingirwa maji.

Amesema watu hao 161 wamefanya idadi ya wasio na makazi katika kata hiyo na kuhifadhiwa  na ndugu na katika shule kufikia 2624.

Amesema vijiji vilivyoathirika ni Mrijo Chini, Kaloleni na Olborot, “Lakini hadi sasa hakuna watu wanaohusika na maafa waliofika kutoa msaada kwa wakazi hawa. Waliotoa msaada ni msalaba mwekundu tu tena wachache.”

“Msaada unaohitajika ni wa mahema, vyakula na mahitaji mengine ya binadamu.”Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.