Header Ads

Akatwa Sehemu za Siri na Mkewe Baada ya Kukutwa na Picha za Ngono Kwenye Simu

Akatwa Sehemu za Siri na Mkewe Baada ya Kukutwa na Picha za Ngono Kwenye SimuWataalamu wa mambo wanasema wivu ni kitovu cha kuimarisha penzi kwa watu walio kwenye ndoa lakini endapo ukizidi unakuwa ni kero na sumu kwa wanandoa, na hilo limethibitishwa kwenye familia ya Azad Singh huko Joginder Nagar mjini Jalandhar nchini India ambapo mzee huyo amejikuta katika hali mbaya kiafya baada ya kukatwa sehemu za siri na mkewe.

Singh (53) alishambuliwa na mkewe kwa kuhisiwa kuchepuka baada ya simu yake kukutwa ikiwa na picha za ngono ambapo mkewe alihisi kuwa picha hizo ni za michepuko yake.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Sukhwant Kaur  (37) amedai kuwa, mumewe usiku wa tukio  alikuwa anaongea na simu na watu ambao hakuwatambua, na baadaye aliposhika simu hiyo wakati mumewe akiwa amelala alikuta kuna meseji za mapenzi kutoka kwenye namba ngeni na picha za ngono ambapo alihisi tayari ameshasalitiwa na ndipo alipoamua kumjeruhi kwa kumkata sehemu zake za siri.

Kwa ripoti iliyotolewa na Jeshi la polisi mjini Jalanddhar imeeleza kuwa mwanamke huyo alichukua hatua baada ya kuripoti kwa muda mrefu kwa ndugu zake kutaka suluhu juu ya tabia ya mumewe ya kumsaliti kwenye ndoa.

“Tulimkamata mwanamke mmoja aliyekuja kuripoti kituoni tarehe 19 Februari 2018 kwa kosa la kumjeruhi mumewe kwa kumkata sehemu zake za siri kwa kisu na kisha kuzidumbukiza chooni, baada ya tukio hilo majirani walisikia kelele na ndipo walipochukua maamuzi ya kumpeleka hospitali ambapo yupo hadi sasa anapatiwa matibabu nahali yake bado ni tete. Sababu kubwa ya Mama huyo kufanya hivyo ni amedai ni wivu wa kimapenzi,  bado jeshi tunaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo,“amesema Kamanda msaidizi wa kituo cha polisi mjini Jalandhar aitwaye Satinder Kumar.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail Mama huyo wa watoto wawili amesema alimvizia mumewe akiwa amelala na kumkata sehemu za siri kisha kuzitumbukiza chooni

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.