Header Ads

Joh Makini Ampigia Simu Mimi Mars Kujua Undani wa Tetesi za Kutoka Kimapenzi

John Makini Ampigia Simu Mimi Mars Kujua Undani wa Tetesi za Kutoka KimapenziWakati stori zikiendelea kuwepo kuwa Joh Makini ana-date na Mimi Mars, rapper huyo mwenyewe ni kitu ambacho kinamshangaza hali iliyopelea kupiga simu kwa muimbaji huyo kujua undani wa tetesi hizo.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Sitamani’ ameiambia Back Stage ya EA Radio wenyewe wanashangazwa na ujio wa taarifa hizo.

“Sielewei maana hata Joh Makini aliniambia Mimi Mars itabidi nikutafute unieleze hizi stori zimetoka wapi, nikamwambia kaka mimi mwenye sijui nimetagiwa tu huko Instagram,” amesema.

“Unajua kuna watu wengine wanaibukaga na stori halafu inakuwa trendig na ninahisi ni kwa sababu watu wajajua ninatoka na nani,” ameongeza.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amesema kwa sasa hatoki na mtu yeyote mara baada ya mahusiano yake ya awali kuvunjika, pia ameongeza kuwa hatarajii kuwa katika mahusiano na mtu yeyote ambaye yupo katika tasnia ya muziki. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.