Header Ads

VIDEO; Waziri: Asilimia Moja ya Watanzania Wagonjwa wa Akili

Waziri: Asilimia Moja ya Watanzania Wagonjwa wa Akili


Licha ya Serikali kueleza kutotambua idadi kamili ya wagonjwa wa akili nchi nzima, inakadiriwa kuwa wagonjwa wa akili ni asilimia moja ya idadi ya Watanzania wote takribani milioni 50.

Akizungumza bungeni leo Februari 6, 2018 Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile ametaja takwimu hizo, kwamba Tanzania itakuwa na wastani wa watu 500,000 ambao ni wagonjwa wa akili.

Amesema  kati ya kadirio la wagonjwa 500,000 ni asilimia 48 tu ndio wanafika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, asilimia 24 wanapelekwa kwa waganga wa kienyeji wakati asilimia iliyobaki wanapelekwa katika huduma za kiroho na wachache ndiyo wanarandaranda mitaani.

Naibu Waziri huyo ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Morogoro

Kusini (CCM), Prosper Mbena aliyetaka kujua ni kwa nini Serikali haina utaratibu wa kuchukua wagonjwa wa akili wanaozunguka mitaani.

“Je serikali inafahamu idadi ya wagonjwa wa akili waliopo barabarani na mitaani kwenye wilaya zote nchini ambao wanahitaji huduma ya matibabu, inatoa maelekezo gani kwa waganga wakuu wa wilaya kuhusu kuwahudumia wagonjwa hao,”amehoji mbunge huyo.

Katika majibu yake, Dk Ndugulile amesema jukumu la kwanza la kulinda afya ya jamii huanzia ngazi ya familia.

Hata hivyo, amekiri kuwa jamii imekuwa ikiwanyanyasa, kuwabagua na kuwatenga wagonjwa wa akili na kusababisha waranderande mitaani.

 “Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria ya afya ya akili ya mwaka 2008 sehemu ya tatu ya kifungu cha sheria namba 9. Inaelekeza kuwa ofisa wa

polisi, ofisa usalama, ofisa ustawi wa jamii, ofisa mtendaji wa kijiji na kata wanalo jukumu la kubainisha mtu yeyote anayerandaranda na kutishia  amani na usalama au kumkamata na kumfikisha sehemu husika,” amesema.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.