Header Ads

Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Aomba kuonana na Raisi Magufuli


   
Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Aomba kuonana na Raisi Magufuli
Tanzania imebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali ikiwemo Tanzanite ambayo hayapatikani nchi nyingine yoyote duniani.

Hata hivyo, Mgunduzi wa madini hayo ya Tanzanite Mzee Jumanne Ngoma amesema kuwa licha ya kugundua madini hayo miaka 52 iliyopita bado hakuna alichonufaika nacho.

Mzee Ngoma amesema kuwa anatamani kuonana na Rais John Magufuli ili amueleze adha anayokutana nayo kwa sababu anaumia kuona hathaminiwi wala kunufaika na chochote licha ya ugunduzi alioufanya.

“Nina mengi ya kumwambia Rais Magufuli kuhusu madini yaliyopo Tanzania mengine ni siri ya nchi siwezi kuyaweka hadharani,” -Mzee Ngoma

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.