Header Ads

PICHA 20: Nyumbani kwa Mtoto Jasiri aliemshtaki Baba yake Polis akitaka kuuza shambaKufuatia clip za video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha mtoto wa darasa la kwanza Antony Petro aliyeamua kumpeleka polisi baba yake mzazi kwa kumsikia anataka kuuza shamba lao, Ayo Tv na millardayo.com zilifika Nyumbani kwao kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Mtoto Antony anazaliwa katika kijiji cha Ngundusi kata Kabanga wilaya ya Ngara mkoani Kagera ambapo kutokana na ujasiri pamoja na hali ambayo sio Nzuri kimaisha, mtoto huyo ulazimika kwenda mtaani kuomba kwa ajili ya kupata chakula cha familia yao, ambapo yupo yeye, dada zake wawili na baba yao.
Mtoto huyo anasoma darasa la kwanza katika Shule ya msingi Ngundusi, na kilio chao Kikubwa wanaomba kusaidiwa anagalau hata kuwapatia sehemu Nzuri ya kuishi Ikiwa ni sambamba na mahitaji muhimu ya binadamu.
Hapo tumekusogezea Picha mbalimbali kutoka kijijini kwao Antony Petro.

Baba alieshtakiwa Poli

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.