Header Ads

KUHUSU HOJA YA KUTOONEKANA KWENYE MATUMIZI YA SERIKALI SHILINGI TRILIONI 1.51.​

Related image
KAULI YA SERIKALI ILIYOTOLEWA  BUNGENI LEO NA NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. ASHATU KIJAJI  KUHUSU HOJA YA KUTOONEKANA KWENYE MATUMIZI YA SERIKALI SHILINGI TRILIONI 1.51.
#Shilingi Tril. 1.51 zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali zimetoka na matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva Tril. 0.6979, Mapato tarajiwa Tril. 0.6873, Mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar Tril 0.2039.
#Mchanganuo huo unafanya jumla ya Shilingi Tril. 1.5891.
#Fedha iliyotolewa zaidi ya mapato (Bank Overdraft) Shilingi Tril. 0.0791 na Fedha zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi ni Shilingi Tril. 1.51.
#Kwa mchanganuo huu ni dhahiri kwamba kwa mwaka 2016/2017 matumizi ya Serikali  yalikuwa makubwa kuliko mapato shilingi Bil. 79.09 ambazo ni overdraft kutoka Benki Kuu ya Tanzani.
#Utaratibu wa kutoa fedha zaidi ya mapato (Overdraft facility) uko kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.
#Kutokana na maelezo haya ya Serikali, napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu na Wananchi kwa jumla kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ipo makini na haiwezi kuruhusu upotevu wa aina yoyote wa fedha za Umma.
#Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuona kwamba, kila mapato yanayokusanywa yanatumika ipasavyo na kwa manufaa ya Wananchi wa Tanzani.
Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO.Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.