Header Ads

Ajali yaua Singida na kujeruhi sita

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa katika ajali iliyotokea mkaoni Singida iliyohusisha gari la halmashauri ya Meatu lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Singida.
Askari Polisi wakiwa eneo la ajali wilayani Ikungi, mkoani Singida.
Akizungumza na www.eatv.tv Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo chanzo chake ni kupasuka kwa tairi la mbele upande wa kushoto.
Gari la halmashauri ya Meatu limepata ajali mkiwa ikungi mkoani Singida likitokea Dodoma, ambalo lilikuwa limebeba watu nane akiwemo  Mkurugenzi wa Meatu pamoja na Madiwani”, amesema Kamanda Magiligimba .
Aidha amewataja waliopoteza maisha kuwa ni aliyekuwa dereva la gari hilo Juma Selemani (38) na  Elias Zakaria ambaye ni Diwani wa kata ya Mwanuzi wilayani Meatu mkoani Simiyu na majeruhi watatu kati ya sita hali zao ni mbaya.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.