Header Ads

Anderson wa Afrika Kusini kumkwamisha Djokovic ?

Mcheza tenisi Kevin Anderson raia wa Afrika Kusini leo anashuka dimbani kucheza mchezo wa fainali ya michuano ya Wimbledon dhidi ya mkongwe Novak Djokovic.
Kushoto ni mcheza tenisi Novak Djokovic wa Serbia na kulia ni Kevin Anderson wa Afrika Kusini.
Mchezo huo ambao utapigwa kwenye 'Centre Court' ya Wimbledon jijini London yenye uwezo wa kuingiza mashabiki ‎14,979 utaanza saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika mashariki.
Djokovic mwenye miaka 31 anaweza kuwa na nafasi kubwa ya kuwa bingwa lakini kutokuwa kwake kwenye kiwango kizuri siku za hivi karibuni ndio kunatia mashaka nafasi yake hiyo kwani hajafanya vizuri tangu alipotwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Ufaransa mwaka 2016.
Kwa upande wake Anderson mwenye miaka 32, atakuwa anasaka ubingwa wa kwanza wa Wimbledon na 'Gland slam' ya kwanza. Hii ndio hatua yake ya juu kuifikia tangu alipofungwa na Rafael Nadal kwenye fainali ya michuano ya wazi ya Marekani mwaka 2017.
Kuelekea pambano hili huenda rekodi na uzoefu ukambeba zaidi Djokovic raia wa Serbia kwani tayari ameshatwaa ubingwa wa Wimbledon mara 3 na Anderson hajawahi. Kevin Anderson anashika nafasi ya 8 kwa viwango vya ubora huku Novak Djokovic akishika namba 21.
 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.