Header Ads

Baba Mzazi Patriki Aongea Mazito Wakati wa Kumuaga Mwanaye " Mimi Ndiye Mume wa Ndoa wa Muna na Baba Halali wa Patriki''


Baba Mzazi Patriki Aongea Mazito Wakati wa Kumuaga Mwanaye " Mimi Ndiye Mume wa Ndoa wa Muna na Baba Halali wa Patriki''
IKIWA ni dakika chache kabla ya kuanza kwa zoezi la kuaga mwili wa mwanaye Patrick, katika Viwanja vya Leaders jijini baba wa marehemu, Peter Zacharia amenyanyuka kwenye kiti chake na kutoa kauli kwa wale waliokuwa wakipindisha ukweli kuhusu uhalali wa yaye kuwa baba wa mtoto huyo.Akizungumza kwa jaziba leo viwanjani hapo, Peter amesema yeye ni baba halali wa Patrick na ni mume halali wa Rose Alphonce Nungu ‘Muna‘ kwani alitoa mahali na wakafunga ndoa, waliishi pamoja na kufanikiwa kupata mtoto kabla ya kuhitilafiana, hivyo watu wanaopindisha ukweli na kusema isivyo kwenye mitandao ya kijamii na kumrubuni Muna waache.
“Nataka niwambie Watanzania mjue, nililipa mahali, nikafanya vikao, tukafunga ndoa na mama mkwe akanikabidhi mwanaye, nafahamu Patrick ametokea wapi, makundi ya kumchanganya huyu hayakunifurahisha hasa wanaomdanganya Rose.“Nimehangaika kuhakikisha namuaga mwanangu pale Mwanyamala, mimi ni maarufu sana lakini sipendi kuonekana kwenye vyombo vya habari, mtoto aliyelala pale (Peter) alinipenda na mimi nilimpenda sana, aliniita Baba Peter, alikuwa akiniombea. Haya yaliyotokea tuyaache. nawashukuru nyote mliokuja kunifarihji, Mungu awabariki sana,” alisema Paba Peter.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.