Header Ads

BARAKA THE PRINCE AHOFIA KUCHANGANYA MASHABIKI WAKE

Add caption
Msanii wa Bongofleva Baraka The Prince amefunguka  kwamba matukio yanayozunguka katika vichwa vya watu kwa sasa ndiyo yamemzuia kutoa wimbo  wakati huu akihofia kuwachanganya mashabiki.
Akizungumza na www.eatv.tv Baraka amesema kuwa hakukurupuka alipotoa tamko kupitia ukurasa wake wa ‘Instagram’ kuwa angetoa wimbo mwisho wa mwezi wa sita, ila hakuweza kufanya hivyo kutokana na sababu zilizo kuwa nje ya uwezo wake.
Huwezi kuambatanisha vitu vya kijamii na burudani,  mfano kama mambo ya kiserikali yanayoendelea na     kombe la Dunia, nitawachanganya mashabiki ngoja haya yapite kwanza nitaachia tu wimbo
mpya
”, amesema Baraka.
Baraka amegusia pia suala la yeye kutoa albamu yake ambayo ni moja ya ahadi zake kwa mashabiki, ambapo amesema kuwa mwezi Disemba ni lazima atoe albam kwani muda wake utakuwa umefika.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.