Header Ads

BASATA yafungukia kuhusu malipo ya wasanii

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limefunguka na kutolea ufafanuzi kanuni zake mpya walizozifanya hivi karibuni kuwa sio kweli kwamba msanii anatakiwa kulipa milioni 5 akifanya tangazo bali kampuni husika ndio inapaswa
kufanya hivyo kwa kuwa wanaingiza kipato kikubwa kutumia tangazo hilo.

Hayo yamebainishwa  Julai 10, 2018 na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza pamoja na Mkuu wa Matukio, Kwerugira Maregesi wakati wakizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo 'PB' inayorushwa kupitia East Africa Radio baada ya kuwepo malalamiko mengi ya wasanii wakidai kanuni hizo mpya haziwatendei haki kwa kile walichokuwa wakiamini kwamba wanapaswa kuilipa BASATA milioni tano kwa kila kazi ya tangazo watakayokuwa wanaifanya na kampuni yoyote ile nchini bila ya kuangalia kiasi wanachokiingiza wao binafsi.
"Hayo makampuni yakifanya matangazo kupitia msanii wanatengeneza fedha nasio kitu cha bure bure tu. Pia hayo makampuni yalikuwa yanafanya kazi na wasanii hao kinyume na sheria bila ya kufahamika na BASATA. Kwa hiyo sasa hivi tutawatambua", amesema Mwingereza.
Pamoja na hayo, Mwingereza ameendelea kwa kusema "milioni tano inalipwa na kampuni husika na wala sio msanii ambaye ametumika kufanya tangazo fulani kwa kampuni".
Mbali na hilo, Mwingereza amesema kuwa sio kweli kwamba walifanya mabadiliko hayo mapya bila ya kuwashirikisha wadau wa muziki kwa kuwa jambo lolote la serikali haliwezi kufanikiwa bila ya kuwepo na maoni.
"Hizi kanuni zisingeweza kutoka kama zisingekuwa na ushirikishwaji, hakuna 'document' ya serikali inayotoka bila ya kuwepo na ushirikishwaji wa wadau. Kuna changamoto ya watu ya kutosema ukweli nchi hii", amesisitiza Mwingereza.
Sikiliza hapa chini viongozi wa BASATA wakiendelea kutoa ufafanuzi zaidi juu ya masuala hayo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.