Header Ads

'Dkt Furaha Mramba' asilimia 34 ya watoto wa Tanzania wanakumbwa na tatizo la kwashakoo

Image result for MTOTO ALIYE KUMBWA NA KWASHAKOO


Imeelezwa kuwa takriban asilimia 34 ya watoto wa Tanzania wanakumbwa na tatizo la kwashakoo na utapiamlo hususani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na Manyoni mkoani Singida.

Mtendaji Mkuu wa wakala wa maabara ya Veterinari Tanzania iliyochini ya wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi,Dkt Furaha Mramba ameeleza hayo jana  jijini Dar  es salaam kwenye mkutano na wanafunzi kutoka Chuo kikuu cha Sydney ambao umefanyika jijini hapa.

Dkt Mramba amesema kuwa kuna haja ya kuwaelimisha  wakina mama namna ya kujikomboa na janga hilo kwani limekuwa changamoto kubwa kwa watoto.

Aidha ameeleza kuwa kutokana na tatizo hilo wameamua kuwafundisha  wanawake njia mbadala ya kufanya ili watoto wao wapate protini ya kutosha.

Wende Maulaga ni Mfanyakazi wa wakala wa maabara hiyo amesema,lengo  lao ni kuhakisha wanashirikiana na taasisi mbalimbali ili kuwezo kutoa elimu kwa jamii kujikomboa na tatizo hilo.

Hata hivyo wanaume wametakiwa kuwaruhusu wake zao kuweza kujiunga katika miradi mbalimbali ya kujifunza namna ya kuwalisha watoto ili waweze kupata ujuzi utakaowasaidia kuepukana na changamoto ya tatizo la utapiamola na kwashakoo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.