Header Ads

Esma Platnumz nampa asilimia nyingi wema kwa mapishi

STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu ana sifa nyingi. Tangu amekuwa staa, mdada huyu anatajwa kuwa mkali sana linapokuja suala la kuigiza hasa ‘scene’ za mapenzi, anasifika kwa shepu lakini pia ni kati ya mastaa wa kike wenye msururu mrefu wa wanaume. Mbali na sifa hizo, Wema anatajwa kuwa kati ya mastaa wa kike ambao wanatisha linapokuja suala la kukaangiza, yaani mapishi. Wapo ambao wanaweza kutoamini katika hili kutokana na jinsi wanavyomuona lakini huo ndiyo ushuhuda kutoka kwa wanaomjua vizuri staa huyu.

Msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni kati ya wanaume walioonja penzi la Wema aliwahi kukiri kwamba, miongoni mwa vitu ambavyo vilimfanya akadumu na mpenzi wake huyo ilikuwa ni suala la mapishi.

“Nimempendea mengi Wema lakini kwa mapochopocho huyu mwanamke ni balaa,” aliwahi kukiri Diamond. Rafiki wa karibu wa Wema, Petit Man naye kuna wakati alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio jijini Dar, aliulizwa kuwa, huwa ni nani anampikia chakula.

Katika kujibu, Petit akasema: “Ni mara chache nakula hotelini lakini huwa nakula nyumbani na wakati mwingine nakula kwa Madam (Wema). Kwa kweli Wema anajua kupika sana, ukienda kwake unakuta msosi wa draft na anakuwa amepika wenyewe.”

Aliyekuwa wifi wa Wema, Esma Platnumz naye aliwahi kusema kuwa, linapokuja suala la usafi kwa mawifi zake waliopita kwa Diamond, Zarina Hassan ‘Zari’ anatisha ila kwenye mapishi anampa asilimia nyingi Wema.
Related image

Sasa, swali ambalo wengi wanajiuliza ni kwamba, Wema kweli anatisha kiasi hicho linapokuja suala la mapishi ama ni sifa za kijinga wanampa? Wanaotilia shaka sifa hizo wanajiuliza kwamba, kwa wana-vyomjua Wema na ule usitaduu wake kweli anaweza kutulia jikoni akasema anapika?

Kutokana na mashaka hayo, mwandishi wetu alimtafuta Wema lakini kwa bahati mbaya simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Mimi nadhani tuwaamini tu wale watu wake wa karibu wanaosema mdada huyu ni mkali kwenye eneo la jikoni. Upishi ni utundu na ule utayari wa mtu kujifunza bila kujali yukoje. Kwa hiyo tukubali Wema yuko vizuri kwenye idara hiyo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.