Header Ads

'Gigy ' mastaa tuliobakia ni mimi na zari

Video vixen na Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameibuka na kudai staa pekee ambaye yupo kwenye level zake ni Baby mama wa Diamond Platnumz, Zari.

Gigy Money amefunguka hayo alipokuwa anaongelea trend yake ya kubadilisha Mawigi na mawiving siku za hivi karibuni.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Gigy amedai yeye na Zari ndio mastaa pekee ambao wanabadilisha nywele kichwani na wengine wote wanakuwa na tabia ya kurudia rudia nywele kichwani.

"Yaani hao wanaojiita mastaa wengi Hawako katika level zangu maana sitaki kufanana nao ndio maana natumia pesa nyingi.

"Hata wewe ukifatilia utajua mademu wanaobadilisha nywele kuna Zari na Gigy na labda nimuweke Irene Uwoya lakini kwa kuwa na yeye ni mtu wa siku nyingi namtoa lakini kwa sasa hivi ni mimi na Zari tu na tunavaa human hair hatuvai plastiki kabisa”.

Lakini pia Gigy Money amedai yeye ni kivutio cha taifa hasa mwili wake umekuwa kivutio kwa wengi ndio maaana anapenda kuchezesha mwili wake na ku twerk Kwenye shoo zake.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.