Header Ads

HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA NJOMBE YAPITISHA JINA LA DIWANI ALIEJIUZURU CHADEMA KUGOMBEA UCHAGUZI MDOGO KATA YA ISAPULANO
Image result for BENDERA YA CCMChama cha mapindunzi CCM mkoa wa Njombe kimetangaza majina ya watia nia ambao watapeperusha bendera katika uchaguzi mdogo wa kata mbili zilizoachwa wazi baada ya madiwani wake kujiuzuri na mwingine kufariki dunia .

Mwanzoni mwa mwaka huu Diwani wa Kata ya Isapulano jimbo la Makete alijiuzuri kwa madai ya kuunga mkono jitihada za rais huku kata ya Itulahumba jimbo la Wanging'ombe likiachwa wazi kutokana na kifo cha ndugu Tito Mdendemi aliekuwa diwani wa kati hiyo.


Akitangaza majina ya wagombea yaliopitishwa na halmashauri kuu ya mkoa katibu muenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole amewataja aliekuwa diwani wa Chadema kata ya Isapulano kabla ya kujiuzuru na kujiunga na chama cha mapinduzi Alphonce Mbilinyi kuwa mtia nia harari kata ya Isapulano huku katika Kata ya Itulahumba Akimtangaza Thobias Mkane.Katika hatua nyingine katibu huyo muenezi amepongeza jitihada zilizochukuliwa na mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka katika kumaliza migogoro ya muda mrefu iliyokuwa ikifurukuta mkoani humo ukiwemo mgogoro wa TRA na wafanyabiashara, Mgogoro wa walimu na halmashauri na Migogoro ya Ardhi.Kampeni za Uchanguzi huyo mdogo unaotarajiwa kufanyika Augost 12 , zinatarajiwa kuzinduliwa mnamo julai 15 na kuhitimishwa Augost 11 saa kumi na mbili jioni huku suala kubwa linalohimizwa ni kufanyika kwa kampeni huru na haki.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.